1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza na Danemark kuondoa majeshi yao kutoka Irak

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPo

Uingereza na Danemark, washirika wawili wakubwa wa Marekani katika vita vya Irak, zimetanga mipango ya kuwaondoa wanajeshi wao kutoka Irak.

Waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, aliliambia bunge la Uingereza kwamba wanajeshi 1,600 watarejea nyumbani katika kipindi cha miezi michache ijayo. Aidha Blair alisema idadi ya wanajeshi watakaorudi nyumbani itategemea ufanisi wa vikosi vya Irak katika kudhibiti usalama.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Danemark, Anders Fogh Rasmussen, ametangaza mpango wa kuwaondoa wanajeshi 460 wa nchi yake kutoka Irak kufikia mwezi Agosti mwaka huu. Hata hivyo Rasmussen, amesema wanajeshi wa Danemark wataendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa vikosi vya Irak.

Matangazo hayo yametolewa huku Marekani ikiendelea kutekeleza mpango wake wa kuwapeleka wanajeshi 21,500 zaidi nchini Irak unaolenga kudumisha usalama katika mji mkuu Baghdad.