1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza yajuta vita vya Falklands

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD7

Huku ikiadhimisha miaka 25 ya vita vya Falklands na Argentina, serikali ya Uingereza imesema inajuta vifo vilivyotokea katika pande zote mbili.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, Margaret Beckett, amesisitiza kwamba Uingereza imejitolea kuwa na uhusiano wa maana na Argentina na akazialika jamii za wanajeshi wa Argentina waliokufa wakati wa vita hivyo zishiriki katika kumbukumbu maalumu visiwani huo.

Mnamo tarehe 12 mwezi Aprili mwaka wa 1982, Argentina ilivivamia visiwa vya Falklands, koloni ya Uingereza kusini mwa bahari ya Atlantic yapata kilomita 600 mbali na ardhi ya Amerika ya Kusini.

Hatua hiyo ilizusha vita vilivyodumu kwa muda wa wiki kumi.