1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Uingereza yakusanya ushahidi wa kifo cha Litvinenko

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpK

Polisi nchini Uingereza leo imekuwa ikikusanya ushahidi juu ya vipi kachero wa zamani wa Urusi na hasimu wa serikali ya Urusi Alexander Litvinenko ameuwawa kutokana na sumu.

Wakati magazeti ya nchi hiyo yakiwa na tuhuma kwamba utawala wa Rais Vladimir Putin unahusika polisi wa kupiga vita ugaidi wanachunguza vipi kiwango kikubwa cha sumu ya miale ya nuklea kutoka madini ya plutonium imeingia kwenye mkojo wa kachero huyo.

Ishara za sumu hiyo pia zimegundulikana kuwepo kwenye sehemu tatu kilabu cha pombe cha Kijapani na hoteli moja ambapo alikutana na watu pamoja na nyumbani kwake Litvinenko.

Litvinenko amefariki hapo Alhamisi ikiwa ni wiki tatu baada ya kuuguwa na amekuwa akichunguza uwezekano wa kuhusika kwa Ikulu ya Urusi katika kuuwawa kwa kupigwa risasi kwa mwandishi habari wa kike Anna Politkovskaya mjini Moscow mwezi uliopita.

Rais Vladimir Putin wa Urusi amekanusha shutuma zote kwamba yeye au serikali yake yumkini ikawa imehusika na kifo hicho cha Litvinenko.