1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Ukungu waendelea kutibua safari za ndege

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCh1

Ukungu bado umeendelea kuugubika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow nchini Uingereza na kukwamisha maelfu ya abiria kwa siku ya nne mfululizo na kuvuruga mipango yao ya likizo.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema ukungu huo unaweza kuendelea hadi siku ya X’masi hapo Jumaatatu.Shirika la Ndege la Uingereza limefuta safari zote za ndani ya nchi lakini zile za nje ya nchi zimekuwa zikiendelea.Uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London na viwanja vya ndege vengine vidogo pia vinakabiliwa na kuahirishwa kwa safari za ndege.

Shirika la ndege la Uingereza limewasafirisha kwa basi abiria 3,000 kwenda viwanja vya ndege vilioko kaskazini mwa Uingereza halikadhalika Paris nchini Ufaransa na Brussels nchini Ubelgiji.