1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Vifo vya watoto duniani vyapunguka

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQ7

Idadi ya watoto wanaofariki kote duniani,imepunguka kwa mara ya kwanza.Kwa mujibu wa takwimu za UNICEF,idadi ya vifo vya watoto ni chini ya milioni 10.Ripoti hiyo inasema, kulinganishwa na hapo awali,sasa watoto wengi zaidi katika nchi zilizo masikini,wananufaika na hatua za kuokoa maisha kama vile kupatiwa nyongeza za Vitamini-A,vyandarua na chanjo.Katika mwaka 2005 vifo vya watoto kote duniani, vilipunguka hadi milioni 9.7 kulinganishwa na milioni 13 katika mwaka 1990.