1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Vikwazo dhidi ya Iran vyafikiwa

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIV

Nchi tano wanachama watano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani zimefikia makubaliano juu ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa kukataa kukomesha urutubishaji wa madini ya uranium.

Vikwazo hivyo ninajumulisha kikwazo cha kuuza silaha katika nchi za nje na kuongezwa kwa sheria za usafirishaji wa fedha za kampuni zinazohusiana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Pendekezo hilo limewasilishwa kwa wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili wajiandae kulipigia kura wiki ijayo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amesema, ´Tunachokifanya ni kuchukua hatua dhidi ya sera kadhaa za Iran nchini Irak na ulimwenguni kote ambazo kwa kweli ni hatari kwa usalama wetu wa kitaifa.´

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amelaani vikwazo hivyo vipya ya Umoja wa Mataifa na ametuma ombi rasmi kwa umoja huo aruhusiwe kulihutubia mwenyewe baraza la usalama.