1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Wabunge wa Uingereza kutoa mbinyo kwa serikali kutamka mkakati wa kujitoa Iraq.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCth

Wabunge wa Uingereza wanamatumaini ya kumlazimisha waziri mkuu Tony Blair kuweza kutoa utaratibu wa mkakati wa kujitoa kwa majeshi ya nchi hiyo nchini Iraq wakati malkia Elizabeth 11 atakapofungua kikao cha bunge wiki hii, magazeti yamesema leo.

Gazeti la Sunday Times na Sunday Express yote yalikuwa na ripoti kuwa wabunge wa kutoka Scotland na Wales watatoa mapendekezo ya mabadiliko katika hotuba ya malkia Elizabeth siku ya Jumatano, inayoitaka serikali kutoa tamko juu ya kuyaondoa majeshi.

Serikali ya Blair imeingia katika uchunguzi mpya kutokana na Uingereza kuunga mkono uvamizi wa Marekani nchini Iraq na kuepuka hivi karibuni kwa kura chache , baada ya bunge kudai kutaka ufanyike uchunguzi wa bunge kutokana na kuhusika kwake katika vita hivyo na matokeo yake.