1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Wanaume wanne wahukumiwa kifungo cha maisha gerezani

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjk

Wanaume wanne walioshukiwa kupanga mashambulio ya mabomu dhidi ya mifumo ya usafiri mjini London Uingereza mnamo mwaka wa 2005, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Wanaume hao walipatikana na makosa juzi Jumatatu kwa njama ya kufanya mashambulio manne ya mabomu mjini London tarehe 21 mwezi Julai mwaka wa 2005, majuma mawili baada ya mashambulio ya mabomu ya Julai saba yaliyofanywa na washambuliaji wa kujitoa mhanga maisha kuwaua watu 56.

Watatakiwa kutumikia angalau miaka 40 gerezani.

Jaji aliyeisikiliza kesi ya washukiwa hao amesema mashambulio ya tarehe 7 na 21 mwezi Julai mwaka wa 2005 yalifanywa na makundi ya kigaidi yenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al- Qaeda.

Peter Clarke, kiongozi wa kitengo cha kupambana na ugaidi mjini London, ameipongeza mahakama kwa kukataa ushahidi wa uongo uliotolewa na washukiwa hao katika juhudi za kukwepa mashataka yaliyowakabili.