1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Washukiwa wa mashambulio ya mabomu wafikishwa mahakamani

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBj

Watuhumiwa watatu wa mashambulio ya mabomu yaliyofanywa mnamo terehe 7 mwezi Julai mwaka wa 2005 wamefikishwa mahakamni hii leo.

Waheed Ali, Sadeer Saleem na Mohammed Shakil, wanashtakiwa kwa kushirikiana na washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga maisha waliokufa katika miripuko ya mabomu mjini London.

Baada ya kuhojiwa kwa mda mfupi na polisi, washukiwa wote watatu wanaoaminiwa kuwa raia wa Uingereza wa asili ya Pakistan, wataendelea kuzuiliwa na polisi hadi tarehe 20 mwezi huu.

Mashtaka hayo ni ya kwanza kuwasilishwa mahakamani kuhusiana na mashambulio ya mabomu ya London dhidi ya mfumo wa usafiri wa treni za chini ya ardhi na basi la abiria.

Washukiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kuripua mifumo ya usafiri na vivutio vya watalii mjini London.

Kamanda wa polisi ya Uingereza, Peter Clarke, amesema kuna uwezekano wa washukiwa zaidi kukamatwa kuhusiana na mashambulio hayo ya Julai saba.