1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Watatu wana hatia.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkO

Mahakama nchini Uingereza imewapata na hatia watu watatu ambao wanatuhumiwa kwa kupanga mashambulizi ya mabomu dhidi ya mfumo wa usafiri mjini London Julai 21 , 2005.

Muktar Said Ibrahim, Yassin Omar, na Ramzi Mohammed wamehukumiwa kwa kula njama ya kutaka kuuwa.

Hukumu kwa watuhumiwa wengine watatu bado inafanyiwa uchunguzi.

Jaji ameliambia jopo la wazee wa mahakama kuwa atakuwa tayari kukubali uamuzi wa wengi wa idadi ya kumi dhidi ya mbili katika kesi hiyo. Mpango huo wa shambulio la bomu ulifanyika kwa wiki mbili kuanzia Julai 7 katika mfumo wa usafiri mjini London , ambapo watu 52 waliuwawa na wengine 700 wamejeruhiwa.