1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Waziri Mkuu Blair aondoka madarakani mwezi Juni

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3J

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair atangatuka madarakani tarehe 27 mwezi Juni.Blair alitangaza hayo Sedgefield,kaskazini mwa Uingereza,eneo analowakilisha bungeni.Aliwaambia wafuasi wake kuwa licha ya mabishano makali yaliyozuka kuhusu suala la kupeleka vikosi vya Uingereza nchini Irak,daima alichukua hatua akiamini kuwa ni hatua iliyo barabara kwa taifa.Risala za kumsifu Blair zimekuwa zikimiminika kutoka sehemu mbali mbali za dunia,serikali ya Bush ikimsifu kama ni “kiongozi wa pekee”.Rais wa Halmashauri ya Ulaya,Jose Manuel Barroso amemsifu Tony Blair kwa jitahada zake za miaka kumi iliyopita kuijumuisha zaidi Uingereza katika Umoja wa Ulaya.Waziri wa fedha,Gordon Brown anatazamiwa kumrithi Blair kama kiongozi wa chama cha Labour na waziri mkuu wa Uingereza.