1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Hali mbaya ya hewa bado yatatiza Ulaya

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfG

Hali mbaya ya hewa imeendelea kuikumba Ulaya ambapo nchini Uingereza zaidi ya familia 250 zimeokolewa katika mji wa chuo kikuu maarufu cha Oxford kutokana na mafuriko mabaya kabisa kuikumba nchini hiyo katika miaka 60 iliyopita.

Katika mji wa Gloucestershire ambao umeathiriwa vibaya na mafuriko hayo zaidi ya watu laki tatu unusu wanakabiliwa na wiki mbili zaidi za kuishi bila ya huduma ya maji safi.

Kwengineko kusini mashariki na katikati mwa Ulaya, joto kali limesababisha vifo vya mamia ya watu pamoja na majanga makubwa ya moto.

Italia na Ugiriki zimeathirika kwa kiasi kikubwa na majanga ya moto ambapo hekari kadhaa zhimeteketea kwa moto kutokana na joto hilo.

Lakini katika milima ya Alps wapanda milima watano akiwemo mjerumani mmoja wamekufa kutokana na baridi kali.