1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Hatimaye Blair asema hadharani Saddam hakutendewa haki wakati aliponyongwa

10 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCc3

Waziri Mkuu wa Uingereza Tonny Blair amesema kuwa utaratibu uliyotumika kunyonga kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein haukuwa sahihi na haukubaliki.

Lakini hata hivyo Tonny Blair amesema kutokubalika kwa utaratibu huo, kusigubike uhalifu wa Saddam.

Hiyo ilikuwa ni mara kwa Waziri Mkuu huyo wa Uingereza kulaani hadharani utaratibu huo, ambapo walinzi walirekodi tukio hilo kupitia simu ya mkononi ikionesha Saddam akipewa maneno ya tashtiti kabla ya kunyongwa.