1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Madaktari wengine kushtakiwa kuhusiana na mashambulio viza !

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBih

Madakari wengine wawili nchini Uingereza na Australia wanakabiliwa na mashtaka kuhusiana na majaribio ya mashambulio katika miji ya London na Glasgow mwezi jana.

Polisi nchini Australia inamshtaki daktari wa kihindi Mohammed Hanaeef kwa kuwasaidia magaidi .

Polisi inadai kuwa kadi ya simu iliyoandikishwa katika jina lake ilikutwa kwa mtuhumiwa mmojawapo.

Daktari huyo alikamatwa na polisi wa Australia wakati alipokuwa anaondoka nchini bila ya kuwa na tiketi ya kurudia.

Na nchini Uingereza polisi ya nchi hiyo imemshtaki binamu wa daktari huyo kwa kushindwa kutoa habari ambazo zingesaidia kuepusha matendo ya ugaidi.