1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Mtandao wa wasafirishaji watu wavunjwa.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD62

Mtu mmoja raia wa Uturuki ambaye amekuwa akiongoza genge la mtandao mkubwa kabisa barani Ulaya wa kusafirisha watu amehukumiwa kwenda jela miaka minane na nusu na mahakama ya Uingereza kwa kuwaingiza maelfu ya watu nchini humo.

Ramazan Zorlu mwenye umri wa miaka 43 amekiri kuhusika kwake na mtandao huo unaohusisha mamilioni ya Euro wa kusafirisha watu, ambao alikuwa akiuendesha pamoja na raia wawili wengine wa Uturuki.

Jaji wa mahakama ya Croydon Crown amesema Zorlu anapaswa kurejeshwa nchini kwake mara baada ya kumaliza kifungo chake.