1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Polisi waimarisha msako

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjj

Polisi mashariki mwa mji wa London wameimarisha msako wa kumtafuta muuaji anae dhaniwa kuhusika na mauaji ya mara kwa mara yanayowalenga wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba.

Katika muda wa wiki moja miili ya wanawake watano imepatikana katika eneo la Suffolk kilomita chache kutoka mji wa Ipswich.

Mauaji hayo yamefanyika katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Konstable Alastair McWhirter wa kituo cha polisi cha Suffolk amesema kuwa mauaji kama hayo hayajawahi kutokea.