1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Rais wa Rwanda akubali uchunguzi wa ndege ya rais wa zamani iliyodondoka

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWT

Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema kuwa anaunga mkono uchunguzi usiopendelea pande yoyote wa ndege ya Rais Juvenal Habyarimana kudondoka na kuchangia kutokea kwa mauaji ya halaiki mwaka 94.Ndege ya Rais Habyarimana ilidenguliwa katika mazingira ambayo hayakueleweka mjini Kigali mwezi Aprili mwaka 94.

Kitendo hicho kilisababisha mauaji ya watu takriban nusu milioni kati ya WaTutsi walio wachache na WaHutu walio wengi.

Uchunguzi unaendeshwa na jaji anayeshughulika na masuala ya ugaidi Jean-Louis Bruguiere kwani wafanyikazi wa ndege hiyo walikuwa raia wa Ufaransa.Jaji Bruguiere anadai kuwa Rais Kagame aliagiza kudenguliwa kwa ndege hiyo ili aweze kunyakua uongozi jambo analokanusha kabisa.

Kulingana na maelezo aliyotoa katika mahojiano na Televisheni ya Uingereza ya BBC Bwana Kagame alisema kuwa hana tatizo na uchunguzi huo kufanyika.