1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London:Uchunguzi wa kifo cha Litvinenko waanza.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpe

Mpelelezi wa Urusi aliyelishwa sumu,Alexander LITVINENKO amefariki dunia.

Wiki tatu baada ya kuutembelea mkahawa mmoja wa mjini London, alikokutana na warusi wengine wawili, sumu aliyopewa imegharimu maisha ya mpelelezi huyo wa zamani aliyekua na umri wa miaka 43.

Waraka alioutoa kabla ya kufariki dunia na kusomwa na rafiki yake mbele ya waandishi habari hii leo mjini London,LITVINENKO anawatwika jukumu la kifo chake viongozi wa serikali ya Urusi.

Mpelelezi huyo alikua mpinzani mkubwa wa rais Vladimir Putin na kabla ya kulishwa sumu, Alexander LITVINENKO alikua akichunguza kisa cha kuuliwa muandishi habari Anna POLITKOWSKAJA.

Wakati huo huo idara ya upelelezi ya Uengereza NEW SCOTLAND YARD inachunguza kisa cha kuuliwa LITVINENKO.