1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London:Uingereza yataka kuwaona awanamaji wake waliokamatwa na Iran.

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFN

Uingereza leo imetaka kuwaona wanamaji wake 15 waliokamatwa na majeshi ya Iran Ijumaa iliopita katika ghuba la uajemi. Maafisa wa Uingereza wamesema hawajui mahala watu hao waliko. Lakini wamesisitiza kwamba walikua katika shughuli zao za kawaida katika eneo la maji la Irak, wakati walipokamatwa. Maafisa wa kijeshi wa Iran wamedai kwamba walipokua wakihojiwa, mabaharia hao waliungama kwamba waliingia katika eneo la maji la iran. Uingereza pamoja na Ujerumani ikiwa mwenyekizi wa sasa wa umoja wa ulaya, zote zimeitaka Iran kuwaachia wanamaji hao mara moja.