1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Uingereza yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEi

Uingereza inatangaza kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Iran kufuatia kutekwa kwa wanamaji na mabaharia wake 15 katika eneo la Ghuba.Waziri wa mashauri y kigeni wa Uingereza Bi Margaret Beckett alitoa tangazo hilo muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Tony Blair kushikilia kuwa itashinikiza nchi ya Iran.

Tangazo hilo linatolewa muda mfupi baada ya maafisa wa kijeshi wa Uingereza kutoa ushahidi ulioonyesha kuwa wanamaji hao walikuwa kilomita tatu nje ya eneo la Iraq walipokamatwa.

Kulingana na msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni Uingereza inavunja uhusiano wake na Iran kwa njia zote zile mpaka suala hilo litatutiliwe.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa wanamaji hao waliingia katika eneo lao bila ruhusa jambo ambalo Iraq inapinga.