1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Wajumbe wa nchi tano za baraza la usalama washindwa kufikia uamuzi juu ya Iran

27 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO9

Wajumbe wa nchi tano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani waliofanya mazungumzo hapo jana nchini Uingereza walishindwa kufikia uamuzi kuhusu hatua za kuchukuliwa juu ya Iran baada ya nchi hiyo kukataa kukomesha mpango wake wa Kinuklia.

Wajumbe hao wanatajariwa kuendelea na mazungumzo yao juu ya suala hilo baadae wiki hii.

Mkutano wa hapo jana ulikuja baada ya shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya Atomiki kuthibitisha kwamba Iran imepuuza muda wa mwisho uliowekwa kusimamisha shughuli zake za kinyuklia.

Muda huo ulimaliza wiki iliyopita.