1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Los Angeles, Marekani. Waislamu wakubali msahama aliomba pope.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD39

Mhariri wa jarida la Kiislamu, amesema kuwa maulamaa na wanazuoni pamoja na Mufti wakuu kutoka mataifa kadha wamekubali hatua ya kuomba radhi ya kiongozi wa kanisa Katoliki Pope Benedikti wa 16 kwa matamshi yake juu ya Uislamu.

Mhariri huyo wa gazeti la Islamica gazeti lililo na makao yake makuu mjini Los Angeles , Marekani amesema kuwa wanazuoni wametia saini barua ya wazi ambayo itawasilishwa kwa balozi wa Vatican.

Mwezi uliopita , Pope alinukuu maelezo yaliyotolewa hapo kale ambayo yanasema kuwa dini ya Kiislamu imekuwa na mambo ambayo ni ya kishetani na yanayokwenda kinyume na ubinadamu.

Nukuu hiyo ilizusha wimbi la mandamano kwa Waislamu duniani kote. Pope baadaye aliomba radhi kwa makosa aliyofanya, na kusema kuwa nukuu hiyo haiakisi maoni yake binafsi kuhusu Uislamu.