1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA: Mafuriko yakumba maeneo ya kusini mwa Afrika.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCY6

Mafuriko yamekumba maeneo makubwa ya Angola, Zambia na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu kiasi hamsini na watano.

Mafuriko hayo yameharibu miji na mazao.

Watu kadhaa wametoweka katika mataifa hayo matatu ya kusini mwa Afrika.

Wakuu wa serikali wametahadharisha huenda kukatokea janga la kibinadamu hasa katika mji mkuu wa Angola, Luanda na maeneo ya karibu ambayo yameathirika zaidi.