1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Chiluba hospitalini baada ya kuzirai

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByf

Rais wa zamani wa Zambia Fredrick Chiluba amelazwa hospitalini baada ya kuzirai hapo jana ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu kuona iwapo ana afya ya kutosha kuweza kukabili kesi ya rushwa.

Msemaji wake Emmanuel Mwamba amesema Chiluba ambaye huko nyuma aliwahi kutibiwa kwa matatizo ya moyo wakati akiendelea kuchunguzwa ameanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa kitandani mwake.

Mwamba ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kwamba madaktari bado wanaendelea kuchukuwa vipimo mbali mbali vya uchunguzi kuyakinisha sababu za kupoteza fahamu kwake.

Chiluba mwenye umri wa miaka 64 alikuwa achunguzwe na madaktari wa Zambia hapo Jumatatu kuona iwapo ni mzima wa afya kuweza kukabili kesi hiyo ya rushwa iliokwama hapo mwezi wa Mei mwaka 2001 kutokana na hali yake ya afya kuwa mbaya.