1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Jumuiya ya SADC yaunda kikosi cha usalama

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYO

Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, imezindua kikosi cha ulinzi kitakachosaidia juhudi za kulinda amani katika kanda hiyo.

Mwenyekiti mpya wa SADC, rais Levy Mwanawasa wa Zambia, amesema kikosi hicho kipya kitashirika katika juhudi za kurejesha usalama na kuwapokonya silaha waasi wakati mizozo ya kivita itakapomalizika katika eneo hilo.

Mkutano wa SADC, unaoendelea Lusaka, Zambia, unamalizika huku waangalizi wakisubiri kwa hamu kubwa ripoti kuhusu juhudi za kuutanzua mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe.

Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa viongozi wa SADC kuhusu juhudi zake

za kumaliza mzozo baina ya chama tawala nchini Zimbabwe, ZANUPF na chama cha upinzani Movement for Democtratic Change, MDC.

Ripoti hiyo ilitarajiwa kuwasilishwa kwa kamati maalumu inayojumulisha wajumbe kutoka Tanzania, Angola na Namibia, ambayo ilitakiwa kuijadili jana mchana, kabla kuwasilishwa kwa viongozi wa SADC wanaohudhuria kikao cha mjini Lusaka.