1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lusaka. Mwanawasa anaongoza uchaguzi hivi sasa.

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD79

Rais aliyeko madarakani nchini Zambia Levy Mwanawasa ameanza kuongoza , wakati kura zikiendelea kuhesabiwa baada ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge, lakini kiongozi wa upinzani Michael Sata amelalamikia baadhi ya matokeo akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu.

Tarakimu za hivi karibuni zilizotolewa kwa ajili ya matokeo ya uchaguzi wa rais na tume ya uchaguzi ya zambia siku ya Jumamosi, zinaonyesha kuwa rais Mwanawasa amepata kura 510,523 mbele ya mgombea wa karibu Sata ambaye amepata kura 473,332 na mfanyabiashara Hakainde Hichilema ambaye amepata kura 441,400.

Sata aliyekuwa akiongoza hapo kabla katika uchaguzi wa rais , amewaambia waandishi wa habari kuwa amegundua udanganyifu katika hesabu ya kura , na ametoa ombi la kurudiwa upya kwa hesabu hiyo ya.

Amesema katika mkutano wa dharura na waandishi wa habari , kuwa hadi sasa amegundua kiasi cha kura 400,000 ambazo zimepotea kutoka katika maeneo ambayo ni ngome yao. Sata ametaka tume ya uchaguzi kutotangaza matokeo rasmi kabla ya kutathmini upya kura hizo.