1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA:Rais Mwanawasa amwonya kiongozi wa upinzani dhidi ya kuunda serikali sambamba

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4P

Rais Mwanawasa wa Zambia amemwonya kiongozi wa upinzani nchini humo Bwana Michael Sata kuwa anaweza kufunguliwa mashtaka ya uhaini ikiwa ataendesha serikali sambamba katika maeneo kama Lusaka na katika jimbo la Copperbelt ambapo mabaraza ya upinzani yalichaguliwa.

Bwana Sata amedai kuwa udanganyifu ulifanyika na kwamba ushindi wake uliibiwa, katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita nchini Zambia.

Kiongozi huyo wa upinzani aliongoza katika hatua za mwanzo za uchaguzi na hasa katika miji mikubwa lakini hakufua dafu katika sehemu za mashambani.