1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA:Wanafunzi wa Chuo kikuu waandamana

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpi

Polisi wa kupambana na ghasia nchini Zambia wamewakamata wanafunzi 49 wa chuo kikuu cha Lusaka. Wanafunzi hao walijaribu kufanya maandamano ya kupinga usafi duni katika chuo chao kwa mujibu wa polisi.Wanafunzi hao walipanga kuandamana hadi majengo ya bunge ili kukutana na waziri wa elimu wanayemlaumu kwa kutotafuta ufumbuzi wa matatizo yao chuoni.

Hapo jana wanafunzi hao walisusia masomo baada ya kufanya maandamano ya kupinga usafi duni.Polisi wa kupambana na ghasia walifunga chuo kikuu cha Zambia na barabara zinazoelekea huko ambako wanafunzi hao walipanga kufanya maandamano.

Maandamano hayo yametokea baada ya usimamizi wa chuo cha Lusaka kuamua kupunguza idadi ya wafanyikazi wa kusafisha mabweni ya wanafunzi kwasababu ya ukosefu wa fedha.