1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG: Umoja wa Ulaya wasita kuiwekea Sudan vikwazo

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7b

Umoja wa Ulaya umeamua kutoiwekea Suda vikwazo kwa jinsi inavyoushughulikia mzozo katika jimbo la Darfur. Mawaziri wa masharui ya kigeni wanaokutana mjini Luxembourg wamesema swala hilo linatakiwa kwanza lijadiliwe na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Afrika Kusini katika Umoja wa Mataifa, Dumisani Kumalo, amesema ni mapema kuiadhibu Sudan kwa vikwazo.

´Nimeshasema na nitarudia tena. Kwetu sisi ni mapema kuchukua hatua dhidi ya Sudan kwa sababu hivi majuzi ilikubali matakwa ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon. Kwa hiyo sielewi vipi vikwazo vitakavyosaidia.´

Wiki iliyopita rais George W Bush wa Marekani alimuonya rais wa Sudan, Omar el Bashir, akisema ana nafasi ya mwisho ya kukomesha mashambulio katika jimbo la Darfur la sivyo akabaliwe na vikwazo na adhabu nyengine.

Sambamba na hayo, mashirika ya kutoa misaada kutoka mataifa ya magharibi yamesitisha kazi zao katika jimbo la Darfrur kufuatia ongezeko la mashambulio dhidi ya wafanyakazi wake. Imekadiriwa watu laki moja wataathiriwa na uamuzi wa mashirika hayo.