1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG:Mawaziri washindwa kuafikiana

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqo

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wamemaliza mazungumzo yao mjini Luxembourg bila ya kupiga hatua katika kuondosha vizingiti vinavyozuia mapatano juu ya mkataba mpya wa mageuzi.

Akizungumza baada ya mkutano huo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank- Walter Steinmeier amesema kuwa hana uhakika iwapo suluhisho litapatikana kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa viongozi wa Umoja huo alhamisi ijayo.