1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa jeshi kutiwa mbaroni Lebanon

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1aQ

BEIRUT:

Jaji nchini Lebanon ametoa amri ya kuwakamata maafisa wa kijeshi 3 na wanajeshi 8 kuhusika na vifo vya waandamanaji 7 wa madhehebu ya Kishia waliopigwa risasi mjini Beirut juma moja lililopita.Jaji huyo pia alitoa amri ya kuwakamata raia 6 waliofanya ghasia na ambao pia walibeba silaha bila ya kuwa na vibali.

Jumapili iliyopita,vikosi vya serikali vilifyatua risasi kuvunja maandamano ya wapinzani waliokuwa wakipinga kukatiwa umeme katika kitongoji cha mji mkuu Beirut.Kama waandamanaji 30 pia walijeruhiwa katika tukio hilo.