1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Raia nchini Senegal wapiga kura kumchagua rais mpya

Lilian Mtono
24 Machi 2024

Raia nchini Senegal wameanza kupiga kura ya kumchagua rais mpya, katika kinyang'anyiro kikali kinachoshuhudiwa baada ya miaka mitatu ya mvutano na mzozo wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4e4Ml
Uchaguzi wa Urais nchini Senegal
Raia wa Senegal akipiga kura katika moja ya vituo vya uchaguzi wa urais katika mji mkuu Dakar, Machi 24, 2024, katika kinyang'anyiro kikali baada ya miaka mitatu ya mzozo wa kisiasa.Picha: Marco Longari/AFP

Karibu watu milioni 7.3 wameandikishwa kupiga kura katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo wagombea wawili wanaopigiwa upatu, Waziri Mkuu wa zamani wa muungano unaotawala, Amadou Ba na Bassirou Diomaye Faye wa upinzani wakichuana vikali.

Mshindi atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal kutoka kwenye changamoto zilizoshuhudiwa hivi karibuni na kusimamia mapato yatokanayo na akiba ya mafuta na gesi ambayo yataanza kuzalishwa hivi karibuni.

Vituo vya kura vinatarajiwa kufungwa saa 12.00 za jioni kwa majira ya nchini humo na matokeo rasmi yakitarajiwa kutolewa wiki ijayo.