1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya Ukimwi yapungua kwa asilimia 17

Thelma Mwadzaya1 Desemba 2009

Leo ni siku ya ukimwi duniani, ambapo Umoja wa Mataifa umeitenga siku hii mahsusi ili kuihamasisha jamii kuhusiana na janga la maradhi hayo ambayo mpaka sasa haya kinga.

https://p.dw.com/p/KmiR
Nembo ya siku ya Ukimwi DunianiPicha: AP

Wakati dunia ikiadhimisha siku hii Nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara, zinaendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliyoathirika na virusi vya HIV, ikiwa ni asilimia 67 ya watu wote duniani wenye virusi hivyo.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi UNAIDS, mwaka eneo hilo la kusini mwa jangwa la Sahara lilishuhudia  maambukizi mapya ya virusi hivyo vya HIV kwa watu  takriban millioni 2, na hivyo kufanya idadi ya watu wanaoishi na virusi hivyo kufikia millioni 22 na laki nne.

Asilimia 60

Karte Welt Infizierte HIV-Fälle in Prozent 2006 Quelle UNAIDS
Ramani ya maambukizi ya mwaka 2006

Wanawake na wasichana ndiyo waliyoathirika sana wakiwa ni asilimia 60 ya idadi ya watu wote walioambukizwa.Afrika Kusini imeendelea kuwa nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi hivyo, ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2007 kiasi cha watu millioni 5 na laki 7 nchini humo wanaishi na virusi hivyo.

Lakini ripoti ya shirika hilo la UNAIDS imeainisha kuongezeka kwa matumizi ya mipira ya kondomu miongoni mwa wanawake nchini humo kutoka asilimia 31.3 mwaka 2001 hadi asilimia 64.8 mwaka jana.

Katika eneo la Afrika Mashahriki , Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi linasema kuwa hali inaonekana kuimarika huku maambukizi ya vuri vya HIV katika nchi za Burundi la Kenya yakipungua.Michel Sidibe ni Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la UNAIDS, alisema kuwa,´´Tumefanikiwa.Ni mara ya kwanza tunaweza kusema kuwa utafiti wetu unaonesha kwamba maambukizi mapya kote duniani yamepungua kwa asilimia 17.Na sehemu kubwa ya mafanikio haya yamefikiwa katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara, ambapo kiwango hicho kilikuwa ni watu laki nne mwaka 2008 tofauti na ilivyokuwa mwaka jana´´

Mabadiliko ya tabia

Kufikiwa kwa mafanikio hayo, kunatokana na kuwepo kwa uhakika wa tiba, ambapo asilimia 44 ya watu wazima na watoto hadi kufikia mwisho wa mwaka jana walikuwa na uhakika wa tiba, tofauti na ilivyokuwa miaka mitano iliyopita ambapo idadi hiyo ilikuwa ni asilimia mbili tu.

Pia kwa mujibu wa shirika hilo, sababu nyingine iliyochangia mafanikio hayo ni pamoja na kubadilika kwa tabia katika ufanyaji wa mapenzi.Hata hivyo Swaziland imeendelea kuongoza  kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ambapo kiasi cha wa millioni moja la kai moja sawa na asilimia 26 wameambukizwa.Kiasi cha watu millioni 14 wamekwishakufa barani Afrika kutokana na maradhi hayo ya Ukimwi, kati ya watu millioni 25 kote duniani.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya-RTRE

Mhariri:Abdul-Rahman