1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maana ya mikutano ya kilele ya nchi za G8

Josephat Charo22 Mei 2007

Mikutano ya kilele ya mataifa ya G8 ilianza kama mazungumzo ya faraghani mnamo mwaka wa 1975. Zikichunguzwa habari zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu mikutano hiyo, ni vigumu kuamini yanayoendelea. Mwandishi wetu Rolf Wenkel, anachunguza vipi mikutano hiyo ilivyokuwa ikiendelea katika miongo iliyopita.

https://p.dw.com/p/CHDw
Waya wa sing´eng´e unaozunguka eneo la mkutano wa nchi za G8 mjini Heiligendamm Ujerumani
Waya wa sing´eng´e unaozunguka eneo la mkutano wa nchi za G8 mjini Heiligendamm UjerumaniPicha: picture-alliance /dpa

Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d´Estaing na kansela wa zamani wa Ujerumani, Helmut Schmidt, waliitisha kwa mara ya kwanza mkutano wa nchi zilizoendelea kiviwanda zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan, Uingereza na Marekani. Wajumbe kutoka nchi hizo walikutana faraghani katika kasri la Rambouillet karibu na mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Mifumo ya kima cha mabadilishano ya fedha ya taasisi za fedha duniani zilizoiidhinisha dola ya kimarekani itumike kama sarafu, zilikuwa zimeporomoka wakati huo, na shirika la nchi zinazosafirisha mafuta duniani, OPEC, lilikuwa limepandisha bei za mafuta duniani kufikia kiwango kikubwa cha kushangaza. Mnamo mwaka wa 1975 viongozi wa serikali sita walitafuta njia ya kuwawezesha kujadili sera za kimataifa kuhusu fedha na kima cha mabadilishano ya fedha.

Kimsingi mpaka leo hiyo ndiyo sababu ya kufanyika mikutano ya mataifa ya G8. Lakini mikutano ya siku hizi inayohudhuriwa pia na Canada na Urusi, si mikutano inayozumguzia maswala ya kiuchumi pekee bali imegeuka kuwa mikutano inayotuwama juu ya siasa za kimataifa na matukio muhimu ya kila siku.

Kila mara kumekuwepo na mada mpya zilizowasilishwa na marais wa nchi na viongozi wa serikali kuhusu sera za maendeleo, kampeni za kuzisamehe madeni nchi maskini, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, ugaidi na uhalifu wa kimatiafa, pamoja na kuporomoka kwa uchumi wa kikanda na maeneo yanayokabiliwa na mizozo.

Shughuli nyingi hufanywa kuandaa kila mkutano wa nchi za G8. Mbali na mikutano ya viongozi wa nchi na serikali, hukutana pia mara kwa mara mawaziri wa mashauri ya kigeni, mawaziri wa fedha, mawaziri wa mambo ya ndani, mawaziri wa mazingira na mawaziri wa maendeleo. Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za mataifa ya G7, yaani nchi zilizoendelea kiviwanda pasipo kuijumulisha Urusi, hukutana mara nne kila mwaka.

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa mataifa ya G7 walikutana mara ya mwisho mjini Denver mnamo mwaka wa 1997 lakini hawakutani tena tangu Urusi ilipojiunga na kuwa mwanachama kamili.

Kimsingi mawaziri huwasiliana mwaka mzima. Vivyo hivyo viongozi wa nchi na serikali huwasiliana kupitia wajumbe wao katika kuandaa mikutano ya kilele ya nchi za G8.

Mjumbe wa Nepal kwa mfano hukutana na viongozi wa kisiasa mara kwa mara kuandaa mkutano wakilele utakaofanyika katika milima ya Himalaya. Huandaa mada, shughuli za kila siku na maamuzi ya mkutano huo, na kazi hiyo inaweza kufanyika kwa haraka.

Kwa mfano hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati wa mkutano wa kilele uliofanyika Genua mnamo mwaka wa 2001, ambapo dola bilioni 1,9 ziliahidiwa kutolewa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na malaria. Makubaliano baina ya serikali mbalimbali yalikuw ayamefikiwa wiki chache kabla ya kufanyika mkutano wenyewe.

Kwa hiyo mikutano ya kilele huwa matokeo ya mabadilishano ya mawazo kuhusu sera kati ya wajumbe. Katika juhudi hizi asasi zisizo za kiserikali, ambazo huchangia mada muhimu, zimekuwa zikihusishwa pia kwa karibu. Asasi hizi zinalalamika kwamba ahado zinazotolewa katika mikutano ya mataifa ya G8 hazifuatwi na vitendo.

Holger Illi msemaji wa wizara ya misaada ya maendeo mjini Berlin hapa Ujerumani, anasema, ili kuweza kutathmini ikiwa nchi za G8 zinatimiza ahadi zao, sharti kufahamu vipi jumuiya hiyo inavyofanya shughuli zake.