1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya ubaguzi Afrika Kusini

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2016

Waandamanaji wamekusanyika nje ya mahakama nchini Afrika Kusini kupinga ubaguzi, ambapo raia wawili weupe wanakabiliwa na mashitaka ya kumshindilia kwa nguvu raia mweusi katika jeneza na kumtishia kumchoma.

https://p.dw.com/p/2SlvD
Südafrika Demo vor dem Gerichtssaal wo Theo Martins and Willem Oosthuizen als Angeklagte sitzen
Picha: Reuters/S. Sibeko

Wanachama kadhaa wa chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress (ANC), na makundi ya upinzani walikusanyika nje ya mahakama huko Middleburg ambako watuhumiwahao walifikishwa mahakamani siku ya Jumatano (Novemba 16).

Vidio inayoonesha tukio hilo la kibaguzi ilisambaa katika mitandao ya kijamii, na kuzidisha mjadala kuhusu athari za historia ya utawala wa Weupe uliohitimishwa mwaka 1994.

Vidio hiyo inamwonesha mwanaume mweusi akijikunyata na kupiga kelele za maumivu wakati mtesaji akiusukuma mfuniko wa jeneza juu ya kichwa chake na kutishia kumwaga petroli kwenye jeneza hilo.

Kesi yao imeahirishwa na itasikilizwa tena Januari 25.