1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano nchini Ukraine

5 Aprili 2007

Maelfu ya wafuasi wa waziri mkuu wa Ukraine, anayeipendelea Russia, waliandamana hadi ofisi ya hasimu wake wa kisiasa, Rais Viktor Yuschenko, wakilalamika kuipinga amri alioitoa ya kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema.

https://p.dw.com/p/CB4t
Maelfu ya wafuasi wa Waziri Mkuu wa Ukraine wameandamana mjini Kiew.
Maelfu ya wafuasi wa Waziri Mkuu wa Ukraine wameandamana mjini Kiew.Picha: AP

Waziri mkuu Viktor Yanukovych katu katu amekataa kuitambua amri hiyo iliotolewa jana, na amesema ataungojea uamuzi wa mahakama kuu ya kikatiba.

Saumu Mwasimba alizungumza na mwandishi wetu katika mji mkuu wa Ukraine,Kiew, Mohammed Masoud, na akamuuliza vipi ilivyo sasa vuta ni kuvute hii baina ya wanasiasa hao wawili ilioanza hata kabla ya mapinduzi ya machungwa ya mwaka 2004 yaliomweka madarakani Rais Yushenko.