1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kudai haki

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Maelfu ya watu waandamana Ujerumani na Uengereza kudai haki sawa duniani

https://p.dw.com/p/HM9A

Berlin/London:


Maelfu ya watu wameandamana mijini Berlin,Frankfurt na London kudai mfumo bora zaidi wa kijamii ulimwenguni.Katika mji mkuu wa Ujerumani,duru tofauti zinazungumzia juu ya waandamanaji hadi 25 elfu walioteremka majiani.Wakipaza sauti "Hatutolipa kwaajili ya mgogoro wenu",waandamanaji hao wamekosoa mabilioni ya fedha ya kuzinusuru benki.Maandamano hayo yameitishwa miongoni mwa wengineo na vyama vya wafanyakazi,mashirika yanayopigania usafi wa mazingira,shirika la ATTAC na vyama cha mrengo wa kushoto.Mwishoni mwa maandamano hayo ya amani,kulizuka machafuko kati ya waandamanaji kadhaa na vikosi vya polisi.Mjini Frankfurt,maelfu ya watu wamedai benki zibebeshwe dhamana ya mgogoro huu wa kiuchumi.Mjini London watu karibu 35 elfu waliaandamana hadi katika mtaa kunako kutikana ofisi za serikali,huko Hyde Park na kulalamika dhidi ya watu kufukuzwa kazini kwasababu ya mgogoro wa fedha na kiuchumi.Mkutano wa kilele wa mataifa 20 muhimu kiviwanda na yanayoinukia-G-20 umepangwa kutishwa alkhamisi ijayo katika mji mkuu huo wa Uengereza.