1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yaendelea nchini Urusi

8 Desemba 2011

Maandamano dhidi ya chama tawala cha Waziri Mkuu wa Urusi, Vladimir Putin na tuhumza za wizi wa kura, kufutia uchaguzi wa bunge jumapili iliyopita yamechemka kwa siku ya tatu mfululizo ambapo polisi nchini humo.

https://p.dw.com/p/13Obe
Members of pro-Kremlin youth movements gather at the Triumphal Square in downtown Moscow, Tuesday, Dec. 6, 2011. Police clashed Tuesday on a central Moscow square with demonstrators trying to hold a second day of protests against alleged vote fraud in Russia's parliamentary elections. Hundreds of police had blocked off Triumphal Square on Tuesday evening, then began chasing about 100 demonstrators, seizing some and throwing them harshly into police vehicles. (Foto:Sergey Ponomarev/AP/dapd)
Waandamanaji UrusiPicha: dapd

Maandamano yaliyofanyika jana katika miji ya Msocow na St.Petersburg yameonekana kutowavutia watu wengi ikilinganishwa na siku zilizopita. Makisio yanaonesha idadi ya waliyojitokeza katika kila mji kufikia 300.

Lakini hali ya Warusi kujitoa kuhatarisha maisha kwa kupotoza muda jela na kupambana na polisi kunaonesha msuguano mkubwa ambao unaweza kuendelea.

Zaidi ya watu 20,000 wametia saini katika kurasa ya mtandao wa kijamii wa facebook ambao unahimiza maandamano makubwa katika Uwanja wa Mapinduzi wa Moscow.

Polisi imeruhusu mkusanyiko huo lakini kwa mashariti ya kutozidi watu 300. Hata hivyo mapokeo hayo yanaonesha dhahiri kwamba yatakuja kuleta sintofahamu na polisi.

Police push people out from a square to prevent a protest against alleged vote rigging in Russia's parliamentary elections in Triumphal Square in Moscow, Russia, Wednesday, Dec. 7, 2011. Protesters energized by the declining electoral fortunes of Russia's ruling party try for a third straight night of demonstrations in Moscow, facing off against a heavy police contingent.(Foto:Ivan Sekretarev/AP/dapd)
Polisi wakikabiliana na waandamanajiPicha: dapd

Chama cha Putin, United Russia kimepoteza sehemu kubwa ya viti vyake katika uchaguzi wa bunge wa jumapili iliyopita ingawa bado kitakuwa na wingi wa viti bungeni. Hata hivyo upinzani unasema hata huo ushindi uliopatikana unatokana na wizi wa kura.

Chama hicho United Russia, kilikuwa na theluthi mbili ya viti katika uchaguzi wa 2007 na kuruhusu kusukuma mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Maadamano haya yanafanyika baada ya rais wa mwisho wa uliokuwa muungano wa Urusi Mikhail Gorbachev kuitaka serikali ya Urusi kuitisha uchaguzi mpya wa bunge na kuyafutilia mbali matokeo ambayo yamekipa ushindi chama cha Vladimir Putin.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimesema kauli hiyo imewafanya raia wengi waamini kwamba matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa ya udanganyifu.

Gorbachev, aliyetawala kuanzia 1985 mpaka 91 baada ya kuporomoka umoja wa kisoviet, ameendelea kupendwa na mataifa ya nje lakini ndani ya nchi hiyo amekuwa akichukuliwa kama mtu asiye na umuhimu wowote.

Wito wake wa kutaka kufanyika kwa uchaguzi mpya utaongeza ari kwa upinzani nchini Urusi lakini utakuwa si lolote wala chochote kwa viongozi waliyo madarakani.

Putin, haoneshi ishara yoyote ya kuwaridhisha waandamanaji. Hapo jana alijisajiri kuwania kiti cha urais kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyia Machi mwakani. Akichaguliwa atakua rais kwa muhula wa tatu.

Mwandishi: Sudi Mnette/APE
Mhariri:Hamidou Oummilkheir