1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yapinga kubakisha majeshi ya Marekani nchini Iraq

P.Martin18 Oktoba 2008

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Iraq Baghdad wakitoa wito wa kuyaondosha majeshi ya Marekani nchini humo.

https://p.dw.com/p/Fca9

Waaandamanaji hao vile vile wanapinga mkataba wa usalama unaotazamiwa kutiwa saini kati ya Washington na Baghdad.

Makundi ya waanadamanaji yalianza kukusanyika tangu Ijumaa usiku kwa maandamano yaliyoitishwa kiongozi wa Kishia Moqtada al-Sadr. Waandamanaji walichoma moto bendera za Marekani pamoja na vinyago vya Rais George W.Bush na Waziri wa Nje Condoleezza Rice.

Hivi sasa serikali za Washington na Baghdad zinajadili mkataba utakaoyaruhusu majeshi ya Marekani kubakia Iraq baada ya mamlaka yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kumalizika mwezi wa Desemba.Sadr na wafuasi wake wanapinga makaubaliano yo yote na Washington yatakayoruhusu majeshi ya Marekani kubakia Iraq.