1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yapinga ubaguzi wa rangi

P.Martin21 Septemba 2007

Nchini Marekani,maelfu ya watu wameandamana katika mji wa Jena,kwenye jimbo la Louisiana kupinga ubaguzi wa rangi.

https://p.dw.com/p/CB16
Wanaharakati wakiandamana kupinga kesi ya wanafunzi 6 weusi wa shule ya Jena,Louisiana
Wanaharakati wakiandamana kupinga kesi ya wanafunzi 6 weusi wa shule ya Jena,LouisianaPicha: AP

Maandamano hayo yamefanywa kulalamika kuhusu mashtaka ya uhalifu yaliyotolewa dhidi ya wanafunzi sita weusi waliompiga na kumjeruhi mwanafunzi mweupe katika ugomvi uliotokea shuleni katika mji mdogo wa Jena.Wanafunzi hao sita weusi wameshtakiwa mahakamani.Wafanya maandamano wanasema,kesi hiyo ni ishara ya sheria inayobagua weusi.

Ugomvi ulizuka baada ya mwanafunzi mmoja mweusi kwenda kukaa chini ya mti ulio katika uwanja wa shule,ambako wanafunzi weupe hukaa.Siku ya pili yake,vitanzi vilining´inizwa kwenye mti huo. Nchini Marekani,kitanzi ni alama inayotumiwa na wabaguzi weupe kuhusika na matumizi ya nguvu.