1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaskofu wajadili hali ya Wakatoliki katika mashariki ya kati

Sekione Kitojo11 Oktoba 2010

Wachungaji hawawezi kusahau hata makundi madogo ya kondoo, na ndipo Jumapili wiki hii ulianza mkutano mjini Vatican unaoangalia hali ya waumini wa kanisa hilo katika mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/PbX0
Pope Benedict 16 anayeongoza mkutano huo wa Sinodi katika makao makuu ya kanisa Katoliki Vatican.Picha: AP

Wachungaji  wakuu   kabisa  hawasau  hata  makundi  yao  madogo ya  kondoo, na  ndipo  siku  ya  Jumapili  tarehe  10 mwezi  wa  huu, ulianza  mjini  Vatican   mkutano  wa  maaskofu  kuangalia  hali  ya waumini  wa  kanisa  Katoliki   katika  eneo  la   mashariki  ya  kati. Kiongozi  wa  kanisa  Katoliki  Benedict  wa  16 anatoa  wito  kwa dini  zote , kuwa  na  maridhiano   pamoja  na  kuwajibika  kisheria.

Mkutano  wa  majimbo  ya  kanisa  Katoliki  kwa  ajili  ya  walio wachache.  Kwa  ajili  ya   kuendelea  kupungua  kwa   waumini. Asilimia  1.6  ya  watu   katika  mashariki  ya  kati  ni  waumini  wa kanisa  Katoliki, ambao  katika   maeneo  ya  mataifa  ya  ghuba wanaongezeka  waumini  hao  kutokana  na   wahamiaji  kutoka bara  la  Asia, lakini  wakati  huo  huo  kutoka  Iraq   waumini  wengi wanakimbia. Hata  katika   nchi  ambayo  ina  waumini  wengi Wakikristo  kama  Lebanon , idadi  inazidi  kupungua  ya  Wakatoliki, analalamika  mchungaji  Tony Cadra.

Tunapaswa  kusitisha  hali  ya  Wakristo  kutoka  katika  dini.  Pia hakuna   mahitaji   ya  vitabu pamoja  na  ushauri.  Tunahitaji mkakati, ili  kuweza  kuendelea  kuwa  na  Wakristo  katika mashariki  ya  kati, kwa  kuwa   hawa  ni  daraja  baina   ya  dini  na mataifa.

Katika  makao  makuu  ya  kanisa  Katoliki,  Vatican  hakuna  mtu anayechoka  kusisitiza , kwamba  sinodi  hii  haina   matokeo  ya lengo  la  kisiasa , badala  yake  ni  kwa  ajili  tu  ya  malengo  ya kiroho. Hata  Pope  Benedict, amerudia  tena  siku  ya  Jumapili katika  mahubiri  yake  wakati  wa  ufunguzi  wa  mkutano  huo. Ndio sababu  anapotoa   miito  yake  mingi   ya  uhuru  zaidi    wa  kidini pamoja  na  kuvumiliana   katika  mashariki  ya  kati  anachukua tahadhari  sana. Benedickt  anakumbuka  wakati  akitoa  mahubiri kwa  lugha  zote  duniani.

Mkutano  huu  wa  maaskofu   wa  majimbo  ni  nafasi  katika  njia  ya kanisa  kuweza  kufufua    imani  ya  Pentekosti  ya  siku  ya kushuka  kwa  roho  mtakatifu,  ili  kutangazwa  habari  nzuri  kuwa huru  na  kuwafikia  watu  wote. 

Siasa  za   busara  pia  ni   mada  nyingine  kubwa  ya  pili  katika mkutano  huu,  siasa  ambazo  hadi  sasa  zimeendeleza  mzozo  wa mashariki  ya  kati. Hapo  kabla  mataifa  ya  Kiarabu  yamekuwa  na wasi  wasi  kuwa  mkutano  huu  unaweza  kutambua  taifa  la  Israel. Katibu  mkuu   wa  mkutano  huo , askofu  mkuu  wa  Croatia  Nikola Eterovic,  ameepuka  mwanzoni  mwa  mkutano  huo  kutaja  upande wowote  pamoja  na  kutaja  jukumu  la  Wakristo  katika  mchakato wa  amani  katika   ardhi  hiyo  takatifu.

Wakristo  katika   mashariki  ya   kati  ni  wanaharakati  wa kupigania   amani  na  wanaoleta  maridhiano,    vitu  ambavyo vinahitajika  sana  katika  eneo  hilo. Wanamatamanio  ya   kuishi kwa  amani   na  majirani  zao  Wayahudi  na  Waislamu.  Kuheshimu sheria   hususan  sheria  za  msingi  za  uhuru  wa  kidini  na  moyo safi.

Mkutano  huu  wa  sinodi  unahuzunishwa  na  athari  zinazotokana na   mzozo  kati  ya  Palestina  na  Israel   na  kuathiri  maisha   ya Wakristo  wengi  Waarabu. Kukaliwa  kwa  ardhi  ya  wapalestina na  Israel  kunafanya  maisha  kuwa  magumu, kuzuwia  uhuru  wa kwenda  watakako,  kuzuwia  ukuaji  wa  uchumi  pamoja  na shughuli  mbali  mbali.        

Mwandishi  :  Kleinjung ,  Tilmann   /  ZR  /  Sekione  Kitojo

Mhariri : Mohammed  Abdul Rahman