1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko katika taasisi za Misaada ya maendeleo

25 Machi 2010

Waziri wa Ujerumani aweka paa moja:GTZ/DED na INWENT

https://p.dw.com/p/Mbvt
Dirk NiebelPicha: AP

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani, Bw.Dirk Niebel,amepiga hatua kubwa katika mpango wake kufanya mageuzi katika sera za misaada ya maendeleo ya Ujerumani. Waziri huyo kutoka chama cha kilberali ,alitoa jana mbele ya Baraza la mawaziri, mpango wake wa kuyakusanya chini ya paa moja mashirika na idara mbali mbali za misaada ya maendeleo.Mashirika hayo ni shirika la Ushirikiano wa Kiufundi (GTZ),Idara ya Ujerumani kwa Maendeleo (DED) na shirika la mafunzo na kujiendeleza kimasomo: (INVENT).

Kwa jumla, idara hizo zote hizo zina watumishi 1.600 katika kila pembe ya dunia.Haraka kuliko alivyotarajiwa, waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani, Dirk Niebel, amepiga hatua mbele kulifanyia mageuzi Shirika la Ushirikiano wa Kiufundi (GTZ) kama alivyopanga.Hii inatokana kwa kuwa tangu awali , alilijumuisha shirika hilo katika marekebisho yake-anaamini hivyo, mwanachama huyo wa Free Democratic Party. Mwanzoni mwaka ujao ,mpango wa kuyakusanya pamoja mashirika ya GTZ,DED na INWENT utaanza n a kwa hatua hiyo nchi zinazo shirikiana na Ujerumani katika sekta ya misaada ya maendeleo zinufaike.Waziri Niebel asema,

"Tunataka Ujerumani,kujitokeza kwa sauti moja-sauti ambayo hata nchi zetu tunazoshirikiana nazo zitaiwezesha kuzungumza na mshirika mmoja na wala sio na wawili au watatu tofauti kuhusu mradi ule ule mmoja .Ndio maana, hatua hii tulioichukua ya kuvikusanya pamoja v yombo hivi vya GTZ,DED na INWENT,ni barabara."

Waziri huyu alieshika madaraka haya tangu mwishoni mwa Oktoba mwaka jana, ana azma ya kukuza uendeshaji kazi ya wizara hii barabara zaidi,kuondosha kuwa na taasisi mbili-mbili.... Misaada ya maendeleo iongozwe na wizara yenyewe na sio kinyume chake-adai Bw.Niebel:

"Hivi sasa hali ilivyo, ni kuwa fikra mara nyingi hutungwa sio na wizara, bali na mashirika yanayo tekeleza miradi.Halafu ndipo, mashirika hayo, yanatoa mapendekezo yao kwa wizara ambayo, huitikia fikra hizo zilizotungwa. Kuongoza kisiasa , ni kutunga mawazo yako na kuyatekeleza kivitendo kwa ushuirikiano na wenzako "

Sawa kama mtangulizi wake katika wizara hii ya misaada ya maendeleo, msocial democrat bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul alieiongoza kuanzia 1998 hadi 2009, Bw.Niebel, anaambatisha umuhimu mkubwa katika kushirikiana katika sera za kimaendeleo.

Usemi kama vile "huyu ni mfadhili" na mwengine ni "mfadhiliwa", ni nadra sasa kusikika.Kwa moyo huu , mwanachama huyu wa FDP anapanga sura moja ya vyombo vya misaada ya Ujerumani, inaeleweka.Shabaha sio kuvipatia viwanda vya Ujerumani masoko zaidi kwa bidhaa zake ,bali ni kushirikiana kimaendeleo.

Mwandishi: Fürstenau (DW Berlin)Uhariri: Josephat Charo