1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko ya tabianchi yanatishia vita dhidi ya Ukimwi

Saleh Mwanamilongo
18 Septemba 2023

Taasisi ya Global Fund inasema mabadiliko ya tabianchi na mizozo duniani vinatatiza juhudi za kimataifa za kupambana na magonjwa matatu hatari ambayo ni Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu.

https://p.dw.com/p/4WSdp
Mabadiliko ya tabianchi yanatishia mapambano dhidi ya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu
Mabadiliko ya tabianchi yanatishia mapambano dhidi ya Ukimwi, Malaria na Kifua KikuuPicha: PongMoji/IMAGO

Ripoti mpya iliyochapishwa usiku wa kuamkia leo na taasisi ya Global Fund inasema mabadiliko ya tabianchi na mizozo duniani vinatatiza juhudi za kimataifa za kupambana na magonjwa matatu hatari ambayo ni Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu.

Ripoti ya taasisi hiyo ambayo ni mfuko wa kimataifa wa kupambana na maradhi hayo, inaonesha kwamba ijapokuwa miradi ya kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu imerejea kote duniani baada ya kuathiriwa na janga la virusi vya korona, lakini hivi sasa inakabiliwa na vizingiti vinavyotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na mizozo.

Mkuu wa Taasisi ya Global Fund, Peter Sands, amesema majanga ya kimazingira mfano wa mafuriko yanaongeza idadi ya wagonjwa na hivyo kuwa vigumu matibabu kuwafikia.

Ongezeko la joto pia limefanya ugonjwa kama Malaria kusambaa hata kwenye maeneo ambayo kabla hayakukabiliwa na  maradhi hayo. Afisa huyo amesema hali inayoendelea sasa inatishia malengo ya kutokomeza magonjwa hayo matatu ifikapo mwaka 2030.