1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko Karachi kati ya wapinzani na wafuasi wa rais Musharaf

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2k

Islamabad:

Wafuasi na wapinzani wa rais Pervez Musharaf wanaripotiwa kupigana katika mji wa kusini mwa Pakistan-Karachi.Polisi wanasema watu wasiopungua 15 wameuwawa na kadhaa wengine kujeruhiwa.Mapigano hayo yamesababishwa na mzozo ulioripuka tangu mwanasheria mkuu alipofukuzwa kazi kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake.Tangu mwezi March uliopita maandamano ya umwagaji damu yamekua yakifanyika dhidi ya rais Pervez Musharaf.Wakati huo huo maandamano makubwa yanatazamiwa kufanyika hii leo mjini Islamabad kumuunga mkono rais Pervez Musharaf.