1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko katika vitongoji vya Paris

Oummilkheir27 Novemba 2007

Jinamizi la mwaka 2005 latishia kuzuka upya katika maeneo wanakoishi wafaransa wengi wenye asili ya kigeni

https://p.dw.com/p/CTgl
Polisi wapambana na vijanaPicha: AP

Machafuko kati ya vijana na polisi katika kitongoji cha Villiers-le-Bel, nje ya mji mkuu wa Ufaransa ,Paris, yameenea hadi katika vitongoji jirani jana usiku..Machafuko hayo yameripuka baada ya vijana wawili wenye asili ya kiafrika kufariki dunia baada ya piki piki yao kugongana na gari ya polisi jumapili iliyopita.

Kisa hicho kinatajwa rasmi kua ni ajali ,hata hivyo uchunguzio unafanywa kujua hasa kilichotokea.

Machafuko haya yanahofiwa yasije yakachukua kipeo cha yale yaliyoshuhudiwa msimu kama huu wa mapukutiko mwaka 2005 katika kitongoji cha Clichy-sous-Bois,karibu na Paris ambapo vijana wawili waliokua wakiwakimbia polisi waligonga mtambo wa umeme na kufariki dunia.Wakati ule machafuko mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa yaliitikisa Ufaransa wiki tatu nzima.

Machafuko ya jana yalikua mabaya zaiidi kuliko yale ya jumapili usiku.Magari,majumba,shule,,mikahawa,maduka na hata maktaba zimetiwa moto.Polisi mmoja anaelezea:

“Vijana wametushambulia-tumejaribu kuwazuwia.Mmoja wao alitufyetulia bunduki.Wenzetu wengi wamejeruhiwa.”

Askari polisi 64 kujeruhiwa, watano kati yao hali yao ni mahtuti.Na watu watano wametiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa mashahidi vijana hao wawili waliouwawa,hawakua wamevaa kofia ya kinga na wao ndio waliosababisha ajali hiyo kutokera.Utafiti umeonyesha polisi wasingeweza kuzuwia ajali isitokee.Vijana lakini wanasema:

“Polisi kila wakati wanatusumbua.Kama si,ku mbili hivi zilizopita walisema“tutakupateni tuu,tunajua vipi.Polisi hawatafanywa kitu,ni watoto wa Sarkozy hao.“

Hali imerejea kua shuwari tangu saa saba za usiku jana kuamkia leo.

Jana familia za vijana hao na viongozi wa serikali ya mitaa walitoa mwito wa subira.Lakini mwito huo haukusikilizwa.Ofisi ya muendesha mashtaka mkuu imeikabidhi idara kuu ya polisi jukumu la kuchunguza kama kuna madai ya„mauwaji yasiyo ya makusudi“ na kutosaidiwa watu ambao waliokua katika hali ya hatari.

Kuna masuala ambayo bado hayakupata jibu licha ya kwamba hoja rasmi zinazotolewa ni kwamba ajali ya barabarani ndio chanzo cha kufariki dunia vijana hao wawili.Masuala hayo ni pamoja na kukawia kufika vikosi vya uokozi au madai kwamba polisi walikimbia ajali hiyo ilipotokea.

Waziri mkuu Francois Fillon amesema amezungumza kwa simu pamoja na wazee wa vijana hao na kuwahakikishia kila kitu kitafanywa kujua hasa kilichotokea.

Waziri wa mambo ya ndani Michele Alliot Marie aliyefika mahala ajali hiyo ilikotokea ame4zusha mjadala mwengine aliposema machafuko ya Villiiers- le- Bel yameandaliwa na baadhi ya watu wanaochochea visa kama hivi kwa manufaa yao wenyewe.

Hoja kama hizo zilitolewa pia wakati wa machafuko ya mwaka 2005 na uchunguzi uliofanywa na polisi na vyuo vikuu umeonyesha machafuko yaliripuka vivi hivi tuu na bila ya kuchochewa na yeyote.