1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko mjini Kampala, nchini Uganda

Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP11 Septemba 2009

Hali ya utulivu imerejea tena katika mji mkuu wa Uganda Kampala baada ya mchafuko ya hapa na pale na mapambano mjini humo kati ya waandamanaji na polisi.

https://p.dw.com/p/JdII
wanajeshi wakishika doria katika mji mkuu wa Uganda,KampalaPicha: AP Photo

Habari zilisema kiasi ya watu saba waliuawa katika ghasia hizo zinazotokana na hasira za wafuasi wa Mfalme Ronald Mutebi wa wabaganda baada ya serikali kumzuwia kulizuru eneo la Kayunga kaskazini mwa Kampala na kusababisha mvutano kati ya Wabaganda na Wabanyala.Nilizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mkaazi wa Kampala Badrudin Khalfan ambaye kwanza alinielezea chanzo hasa cha mfutano kati ya Wabaganda na Wabanyala na kama kuna mkono wowote wa kisiasa.