1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko nchini Nigeria, 300 wameshakufa.

Abdu Said Mtullya30 Julai 2009

Watu 300 wameshakufa kutokana na mapigano nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/IzuI
Rais Umaru Yar'Adua amesema majeshi ya serikali sasa yanadhibiti usalama nchini Nigeria.Picha: AP

MAIDUGURI.

Polisi nchini Nigeria imesema watu zaidi ya 300 wameshauawa kutokana na mapambano ya siku nne baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la kiislamu, kaskazini mwa Nigeria.Maalfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mapigano hayo.

Maafisa wa serikali wamesema mapigano hayo yapo hasa katika mji wa Maiduguri, ambao ni makao ya kundi hilo linaloiga mfano wa taliban. Kundi hilo linapigania kutumiwa kwa sheria za kiislamu nchini Nigeria kote.

Rais Umaru Yar'Adua ameliagiza jeshi kuwazima waislamu hao mara moja.