1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapeleka wanajeshi kudhibiti machafuko

14 Juni 2010

Zaidi ya watu 117 wameuawa, 1000 wamejeruhiwa

https://p.dw.com/p/NqF5
Hali bado ni tete nchini Kyrgyzstan.Picha: DW

Vita baina ya makabila ya Wahuzbeki na Wakirgiz nchini Kyrgyzstan vimezidi kuzusha hofu kwa wakaazi wa nchi hiyo huku ikielezewa kuwa idadi ya watu ambao wameshafariki kufikia 117,na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa.

Kutokana na Kyrgyzstan kuwa ni ngome muhimu kwa kambi za kijeshi za Marekani na Urusi,imeilazimu Urusi kuitikia haraka wito uliotolewa na Rais wa muda wa nchi hiyo Roza Otunbayeva kuitaka nchi hiyo kupeleka majeshi nchini humo ili kudhibiti machafuko hayo.

Hali ya usalama imeelezwa kuzidi kuwa mbaya,kutokana na jeshi dhaifu la nchi hiyo,ambapo Urusi imeshapeleka majeshi yake nchini humo katika kambi yake ya kijeshi ilioko katika mji wa Kant.

Serikali ya muda nchini humo,imeituhumu familia ya Rais aliyekimbilia uhamishoni Kurmanbek Bakiyev kuhusika na machafuko hayo makubwa ya kikabila.

Naibu kiongozi wa serikali ya muda ya Kyrzgystan Temir Sariyev amewaambia waandishi wa habari kuwa,kuzuka kwa mapigano hayo nchini humo,kumelifanya jeshi la nchi hiyo kushindwa kuidhibiti hali hiyo.

Hali imeelezwa kuzidi kuwa mbaya kufuatia makundi ya watu wa kabila la Wakirgizi kuanza kuyashambulia maduka na nyumba za wakaazi wa kabila la Wauzbeki,makabila ambayo ni makubwa nchini humo.

Kufuatia hali ya mashaka kuongezeka nchini humo,Serikali ya China imesema kuwa leo itatuma ndege yake nchini humo,kwa ajili ya kuwanusuru raia wa nchi hiyo ambao wamejikuta wanatumbukia katika tafrani hiyo,ambapo Serikali ya muda ya Krgyzstan imeeleza kuwa inaendelea na zoezi la kupeleka misaada ya chakula iliotolewa na shirika la afya ulimwenguni,Urusi na nchi ambazo hazikutajwa.

Kufuatia hali hiyo,msemaji wa siasa za nje kutoka Umoja wa ulaya,Catherine Ashton ameelezea kufadhaishwa kwake na matukio ya machafuko hayo,ambapo amefafanuwa kwamba ameshafanya mazungumzo na Urusi na Jumuiya ya usala na ushirikiano barani Ulaya (OESE),ili kutafuta namna ya kudhibiti machafuko hayo.

Wananchama wa ushirikiano wa pamoja wa kijeshi unaozijumuisha nchio saba zilizokuwa zamani sehemu ya Muungano wa Kisovieti, ambapo Kyrgystan ni mwanachama zinapanga kukutana mjini Moscow, kuzingatia hatua za kuchukuliwa kurejesha amani katika taifa hilo la Asia ya kati.

Mwandishi; Ramadhan Tuwa/DPAE/AFPE/APE

Mhariri;Abdul-Rahman,Mohammed