1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yametulia kidogo nchini Ufaransa

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUcy

Paris:

Hali ni tulivu kidogo katika kitongoji cha Villier le Bel karibu na mji mkuu wa Ufaransa Paris.Mamia ya polisi waliwekwa jana usiku kuzuwia machafuko.Hata hivyo visa vya hapa na pale vimeripotiwa ikiwa ni pamoja na kutiwa moto madebe ya taka na magari katika kitongoji hicho ambako vijana wawili waliuwawa jumapili ilioyopita,piki piki yao iliüpogongana na gari ya polisi.Polisi zaidi ya 120 wamejeruhiwa na vijana waliokua wakiwapiga mawe na bunduki .Rais Nicolas Sarkozy ameamuru uchunguzi huru na wa kina ufanywe na kuahidi pia waliowahujumu polisi watafikishwa mahakamani.Rais huyo wa Ufaransa amelihutubia taifa hii leo.