1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yazuka Senegal

28 Januari 2012

Machafuko yametokea katika mji wa Dakar nchini Senegal, baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kuamua kwamba kisheria, rais wa sasa Abdoulaye Wade anaweza kushiriki katika uchaguzi wa mwezi ujao, kugombea awamu ya tatu.

https://p.dw.com/p/13sFo
United Nations soldiers from Senegal patrol in the streets of Abidjan, Ivory Coast, Thursday, Dec. 9, 2010. The U.N. Security Council is ready to take targeted measures against people who try to upset the peace process or violate human rights in Ivory Coast. The international body is also calling on all sides to respect the electoral victory of opposition presidential candidate Alassane Ouattara. (AP Photo/Thibault Camus)
Walinzi wa amani Senegal 2010Picha: AP

Waandamanaji waliwarushia mawe polisi ambao walijibu kwa kufyatua mabomu ya machozi huku kukiwa na ripoti ya kifo cha polisi mmoja.

Shirika la habari la Reuters limesema, maripota wake wamewashuhudia vijana wakichoma moto matairi na kupindua magari, baada ya uamuzi huo kutolewa jana jioni. Wapinzani wa Wade mwenye umri wa miaka 85 wamesema, katiba hairuhusu kushika wadhfa wa urais kwa zaidi wa mihula miwili. Wade alieshika madaraka 2000 na kuchaguliwa tena 2007, amesema, awamu yake ya kwanza ilikuwa kabla ya mageuzi ya katiba ya mwaka 2001 yaliyoweka kiwango hicho.

Mahakama Kuu imewaidhinisha wagombea wengine 13 lakini wamepinga ombi la muimbaji maarufu Youssou N´Dour anaetaka kugombea urais. Kwa mujibu wa mahakama muimbaji huyo hajakusanya saini 10,000 zililizothibitisha kumuunga mkono, kama inavyohitajiwa.